Home GENERAL Bachela Lyrics – Queen Darleen Ft Lava Lava – New Song 2020

Bachela Lyrics – Queen Darleen Ft Lava Lava – New Song 2020

by Louis
Published: Last Updated on
Bachela Lyrics

Bachela Lyrics – Queen Darleen Ft Lava Lava – Download Mp3 Audio

Verse One

Eti Lava utaoa lini
Mbona unazingua
Wazuri wengi mjini
Wezi wanachukua

We kutwa ubishoo
Nywele kuchange mitindo
Wanakuona wafoo
Kila siku uko single

Moyo wa kupenda sina
Ya nini nijipe homa
Si huyu ni mwana Stamina
Rafiki yake Roma

Si unajua ndoa majaliwa
Nasubiria apange Maulana
Atanitunukia
Bado naula ujana

Ujana maji ya moto
Utakuunguza utakuunguza
We pita peku mpoto
Tutakuuguza

Kwanza kuolewa raha
Oh na na wili wili
Ona mume wangu hii spa
Atumiliki wawili wili

Umenikumbusha kule Insta udaku
Wanasema mume umekwara
Ati umefuata hela
Ukakubali kuolewa mitara

Utanishauri mimi, wakati wangu ndo sasa
Mimi mtoto wa mjini
Kula beer shida chini, acha nile bata
Nijipe stress za nini

Chorus

Bora niwe bachela
Sitaki kujifunga funga, kujibana bana
Niwe bachela, kwanza naona mapenzi
Faida hayana
Bora niwe bachela eh

Huo ni utoto unajidanganya
Niwe bachela
Unayoyafanya mwisho hayana
Bora niwe bachela!

Verse Two

Dada Darleen acha kunichachafya
Uliza kilomkuta Dangote
Sijui kangombana na Tanasha
Ametu unfollow wote

Mapenzi ya siku hizi
Shemeji Lokole mwongoza umbea
Mkigombana tu kashatizi
Insta nzima yameshaenea

Ndio maana nimetulia
Navuta pumzi staki kwenda mbio
Mambo ya kujifanya hodari eti mjuzi
Ujuzi huo kwio

Tukiachana na yote
Mimi bado sikuungi mkono
Wasafi wote
Mnaonekana mnapenda ngono
Duu

Utanishauri mimi, wakati wangu ndo sasa
Mimi mtoto wa mjini
Kula beer shida chini, acha nile bata
Nijipe stress za nini

Chorus

Bora niwe bachela
Sitaki kujifunga funga, kujibana bana
Niwe bachela, kwanza naona mapenzi
Faida hayana
Bora niwe bachela eh

Huo ni utoto unajidanganya
Niwe bachela
Unayoyafanya mwisho hayana

Mabachela piga kelele, Weee
Piga kelele moja, Weee
Kelele mbili, Wee wee
Piga kelele tatu, wee wee

Wenye wapenzi piga kelele, Wee
Walio oa, Weeee
Tulio olewa je, Wee wee

Abby Daddy

Bachela Lyrics Credit – Queen Darleen and Lava Lava

ALSO, SING TO – Daktari Lyrics by Wyse New Song March 2020

Related Posts