Home GENERAL Daktari Lyrics by Wyse New Song March 2020

Daktari Lyrics by Wyse New Song March 2020

by Louis
Daktari Lyrics by Wyse

Contents

Daktari Lyrics by Wyse – Download Mp3 Audio

Verse One

Uzuri wako asumini
Asumini napenda ukichanua
Mizunguko kama feni
Feni bovu chumbani wanipepea

Una maadili, umefunzwa umefunzika
Sifa wastahili, kwako nafaidika
Sihitaji darubini, darubini
Mazuri kukupimia

Hawajui unayonipa mie
Penzi lako maridhawa
Oooh hawajui acha nining’inie
Mapigo yangu ya moyo we ndo dawa

Chorus

Daktari wee, daktari
Unajua dozi yangu
Daktari wee, daktari
Ooh watibu maradhi yangu
Daktari wee, daktari
Bingwa wa hisia zangu
Daktari wee, daktari
Basi nipe mambo yangu

Verse Two

Nikichechemea unaniriwaza
Unanipa nguvu ya kuamka kesho
Unanipokea na vizawadi vidogo vidogo
Vyote kwako wewe ni special

Nimegubikwa na furaha, nyota yangu inang’aa
Pete yangu umevaa usiivue
Usijekukata tamaa, vijineno vya mtaa
Ukajikuta umevivaa usinitue

Hawajui unayonipa mie
Penzi lako maridhawa
Oooh hawajui acha nining’inie
Mapigo yangu ya moyo we ndo dawa

Chorus

Daktari wee, daktari
Unajua dozi yangu
Daktari wee, daktari
Ooh watibu maradhi yangu
Daktari wee, daktari
Bingwa wa hisia zangu
Daktari wee, daktari
Basi nipe mambo yangu

Oooh oooh, ayee eeh
Sasambu sasambua, Sasambu sasambua
Sasambu sasambua mama wee

Oooh oooh, ayee eeh
Sasambu sasambua, Sasambu sasambua
Sasambu sasambua mama wee

Daktari Lyrics by Wyse

ALSO, SING TO – Basi Lyrics – BONGA – New Song 2020

Related Posts