Home GENERAL Kaka Tuchati Lyrics – Rostam

Kaka Tuchati Lyrics – Rostam

by Louis
Kaka Tuchati Lyrics

Contents

Rostam Kaka Tuchati Lyrics

Kaka Tuchati Lyrics Verse One

Ooii naona mkandaa unakatika
Uko kimya sana mkato au kundi limevunjika
Na utanyooka raundi hii
Na hivi huwezi bila mimi?

Najikuta JAY Z oya unarudi lini?
Kaka, huku wamefunga mipaka
Ila tiketi nilikata nirudi kabla pasaka

Rudi ugeuze kisu sio
Mwana kulitafuta mwana kulipata
Raundi hii sio ununio
Daraja la ,,,,

Basi kumekucha
Ni saa ngapi huko nipe takwimu
Nimeamka nishaweka bundle
Namwongoja Ummi Mwalimu

Anapambana yule dada
Tanga nimewavulia kofia
Wametoa sanitizer za iliki
Yaani ukipata unalipia

Corona nishai
Yaani bongo kila mtu daktari
Maasai kachemsha majani
Ya mpapai kanywa na sukari

Buza hadi maski wanafua
Sijui nani kawafundisha
Huku kuna dada kajifukiza
Mashetani akayapandisha

Tueke siasa kando
Unajuwa uchumi unashuka?
Sio bongo tu hadi ng’ambo
Watu wamefunga maduka

Hapa nawaza pesa ya pango
Benki waliokopa wanajuta
Tukisema tukae ndani
Na hii njaa si tutakufa?

Hali inatisha na umaskini
Tunaoumia ni sisi
Yaani bora ufe kwa ukimwi
Angalau utaandika urithi

Kwa hiyo hamna bata
Sio kidimbwi sio tipsi
Kaka madanga wamekata
So hazitimbi hizo pisi

Chorus

Bwana wa mabwana
Mungu wa miungu
Alpha na Omega
Nani kama wewe?

Bwana wa mabwana
Mungu wa miungu
Alpha na Omega
Nani kama wewe?

Kaka Tuchati Lyrics Verse Two

Hivi unakaa jimbo gani
Au Marekani ya vijijini
Unajikinga vipi maana
Vifo vingi hadi siamini

Mmm au umesharudi
Uko zako rohoro nini?
We bana ebu niache
Mi nimeze Chloroquine

Umenikumbusha
Kwani Chloroquine ni dawa?
Bado inafanyiwa uchunguzi
Ila haijathibitishwa

Ingawa ukinywa Haitatarisha
Ndio maana bado wanaigawa
Mi nakunywa maana
Nilishika uso kabla ya kunawa

Eti unaweza kawa nayo
Na usionyeshe dalili?
Ewaa, uko sahihi

Na kingine kuhusu hili
Ni kwamba mgonjwa wa corona
Unaweza usimtambue kwa macho
So mtu yeyote unamwona
mpe mita mbili toka kwako

Na hiko kifanslika
Ndio kinini baba Willy?
Ni Ventilator ni machine
Ka mapafu ya nje ya mwili

Sijaelewa, embu nieleweshe
Kuhusu hili, nasikia vinauzwa ghali
Basi vile vingi mwimbili

Okay, kirusi cha corona
Kinashambulia mapafu
Ndipo zinaanza homa, mafua ya kifua

Halafu unashindwa kupumua
Na mwili unahitaji dafu
Ventilator huingiza hewa
Na kuitoa iliyo chafu

Tuepuke mikusanyiko
Ikibidi tukae ndani
Tumeambiwa tujifukize
Hivi ni dawa unadhani?

Ngoja kwanza
Hivi fumigation
Mmm mmm
Baba ile inaua mende
Acha utani

Chorus

Bwana wa mabwana
Mungu wa miungu
Alpha na Omega
Nani kama wewe?

Bwana wa mabwana
Mungu wa miungu
Alpha na Omega
Nani kama wewe?

Verse Three

Maisha ya upweke yanasumbuwa
Ila siku zinapita
Yule mkewe itunze pete mtayamaliza
Na uhakika kaka

Ila hatua dua
Haina haja ya kusikitika
Ila navyokujua
Kweli hujazini miezi sita

Kiukweli mi mwaminifu
Ingawa jogoo anawika
Mama Ivanny mabalifu
Hakuchiti una uhakika?

Kuna mchezaji wa yanga
Namuona anapita pita
Nitamkata kata mapanga
Yaani namuua na namzika

Oyah wape nyumbani
Basi pesa ya matumizi
Kaka nitoe wapi
Na show hakuna sikuhizi

Hali imekuwa ngumu
Hakuna pesa kila corner
Kila mtu unayemdai
Naye anasingizia Corona

Mbona sasa wanafunga shule na vyuo
Halafu bar hawafungi
Mzazi atamlindaje mtoto
Na akirudi na akirudi yupo tungi

Polisi India wanapiga watu wakisongamana
Wao wabarakoa wanajua hadi fender wamebanana
Sasa wanatukusanya kutuambia tusikusanyike
Ila wauguzi wanajitoa sana
Duh, Mungu awalipe

Wapinzani mnatangaza vifo
Walopona hamwatangazi
Wanasema mungeeka takwimu
Za wazi ingekuwa kizazi

Kwa hiyo lockdown hakuna
Halafu umeona texti niliotuma?
Ipi? kwenye group
Mbona inbox hakuna?

Nasikia, nini?
Kwa Yuzee Kambochi
Maana huko uliko usiongee
Sana inatosha

Hadi papai lina Corona! duh
Kaka Tuchati
Mmm na mbuzi vipi?
Ee eh Kaka Tuchati

Mwili umekufaa ganzi
Kaka Tuchati
Poa mwanangu tundelee kujifukiza

Rostam Kaka Tuchati Lyrics

ALSO, SING TO – Kiwembe Lyrics – Joh Makini Ft Lady Jaydee

Related Posts