Home NEWS Mkombozi Lyrics – Roma ft One Six – New Song Jan 2020

Mkombozi Lyrics – Roma ft One Six – New Song Jan 2020

0
Mkombozi Lyrics

Mkombozi Lyrics – Roma ft One Six

Mkombozi Lyrics Verse One – Roma

Napiga goti napiga ishara ya msalaba
Dunia imenipiga kofi namuomba baba la baba
Nipimie shoti la bapa nizime mada
Asubuhi nigongee noti niende kuifanya ibada

Nadaiwa kodi ya pango nadaiwa ada ya watoto
Na mama wa kambo anamchuna baba
Na baba yuko ng’ambo ni mwaka sijaona msaada
Ama kweli dunia ina mambo hadi jogoo anaweza taga

Jirani ananiambia be humble
Be humble kipiga kizinga unafunga mlango
That’s ridiculuos haha its now funny am serious
Am genius though inanitesa am notorious

Baba hakutupa urithi wapasi wala feni
Wala peni ambayo ingenipa elimu shuleni
Bali alituachia madeni na sifa ambayo  ya kweni
Sasa huyo ndo baba gani humble au mtemi

Na mtaani kuna denti nimempa mimba
Mtoto wa mjeda muda wote pira litadimba
Na sina dusko so kwa doctor siwezi timba siwezi vimba
Na kina chocho mbogo wananiwinda

Chorus

Nimekesha kwa waganga
Nimevunja nazi njia panda
Nimeshikishwa tungule msata mkata
Nikabeba manyanga

Mikesha kinabiiii
Nyumba zote za ibada
Nimeshiriki sana
Maana sura kukufura si jangwa nawe

Kumbe yupo mungu mkombozi
Wa kukufuta machozi pale unapolia mwana we baba
Kumbe yupo mungu mkombozi
Wa kukufuta machozi pale unapolia mwana we baba

Mkombozi Lyrics Verse Two

Nishaiba nikaenda mabusu na ndugu hawakuja niona
Na wakasema hayawahusu mwizi anatakiwa kuchomwa
Nilipotoka nikawabusu wakasema nimewasonya
Nikaona eeeh maji mazito kuliko damu ya roma

Ukiendekeza ndugu utavuna magugu
Utakufa kidudu na mungu hutamwabudu
Utamkataa wa joto utamkana wa baridi
Atabakia wa vuguvugu naye pia ataleta gubu

Sikampiketo stressi  inaleta karaha
Freshi be passion anguko kubwa ni kuikosa attention
Its not fair nawapa popodho they dont care
Na watasema huna demandi fitina watakuekea

Huku nadaiwa vikoba kule nadaiwa rejesho
Naenda kujificha goba usiku narudi peko
Nawaza hata kuroga nikiamini nitaipata kesho
Au lizari sala toba nijue nikwepe mateso

Ooh Jesus fanya miujiza
Naona giza ukija mwanga Unaniumiza
So please kama unaskiza naijongea hatari
Useme neno moja tu naahidi nitakesha pale

Chorus

Nimekesha kwa waganga
Nimevunja nazi njia panda
Nimeshikishwa tungule msata mkata
Nikabeba manyanga

Mikesha kinabiiii
Nyumba zote za ibada
Nimeshiriki sana
Maana sura kukufura si jangwa nawe

Kumbe yupo mungu mkombozi
Wa kukufuta machozi pale unapolia mwana we baba
Kumbe yupo mungu mkombozi
Wa kukufuta machozi pale unapolia mwana we baba

We baba we mwana
Aah pale unapolia mama eeh eee eee
Kumbe yupo mungu mkombozi
Pale unapolia mama we baba
Kumbe yupo mungu mkombozi
Pale unapolia mama we baba

Credit: Roma and One Six

ALSO, SING TO: Kata Lyrics – Ommy Dimpoz ft Nandy – New Song 2020

Leave a Reply