Home GENERAL My God Lyrics – Nacha

My God Lyrics – Nacha

by Louis
Published: Last Updated on
My God Lyrics by Nacha

My God Lyrics by Nacha – Download Mp3 Audio

Verse One

Mungu wangu narudi kwako mi ni mwanao
Ni mkosefu sijakamilika
Na sihitaji kuwa kama wao
Napiga goti nikiwa nimechoka
Nilikosea wapi nisahihishe upya
Maana wenzangu wanapata mimi nakosa

Tazama nilivyo mnyonge na mwenye shauku kubwa ya kufanikiwa
Masikini mwenye ndoto nyingi za kusadikika zisizofanikiwa
Mungu wangu haujawai kushindwa kama uliweza kufanya masika na kiangazi
Basi unaweza ukafanya na mimi pia nikapata kazi

Mungu wangu nivalishe nguo maana walimwengu wamenivua
Tena bila haya nayasema haya nikiwa na akili timamu natambua jema na baya
Wamenitupa kwenye jua niungue, kwenye mvua nilowane
Nishushie muvuli wako wafadhaike Mungu wangu na watukane

Nifanye ning’are na nisihadaike nikavimba
Mi ni mende tu ila nifanye kila wakiniona wanione simba
Mungu kama ulinileta duniani nikiwa nalia
Ni wazi ulitaka kunionesha dunian ni mbaya
Na walimwengu ni wabaya hawana haya
Na ndio maana nayasema haya

Walishanitupia mawe na kunitishia uhai
Nikawaambie sihofii
Nikawaambie nina mungu wangu anayenilinda
Kwa hiyo wala sijutii

Nikawajibu namsikia mungu tu
Nyinyi wasaliti vigeugeu wanadamu siwasikii
Wakanicheka sijapata nikawaambia hizo zote kudra
Mungu wangu ananipenda hanichukii
Na nikawajibu nitapata muda ukifika
Sababu mungu wangu hawahi wala hakawii

Verse Two

Mungu, duniani hakuna haki
Mwenye mabavu ni mabavu
Na mnyonge ni mnyonge
Hakuna usawa wala haki

Mungu wangu hujaziba masikio unanisikia
Huwa nageuza maneno yao machafu
Kuwa masafi na kisha nawarudishia
Labda mimi ni mshamba sana
Sijui kuvaa wenyewe wanaita fashion

Sipati michongo nimezubaa sana
Wenyewe huiita connection
Natamani na mimi siku moja nipate
Nisahau kuhusu maumivu

Na nafanya kazi usiku na mchana
Sio kwamba mimi ni mvivu
Mi ni baba wa familia
Na niko na mke na watoto pia

Mi ndio muhimili nikilala njaa
Wamelala njaa na wao pia
Mungu tazama mi ndio baba mi ndio mama
Na hakuna kipato

Marafiki niliowaomba msaada
Waliishia kunijibu kila mtu atakula kwa jasho
Nyumbani dada yangu chausiku ni mgumba
Na anatamani mume na hajapata
Na wakati muda huo huo jirani alibarikiwa mtoto na anamtupa

Mungu wangu wainuwe wanawake wanaosalitiwa
Na kuonewa wanaume zao
Wanaoteseka na mapenzi wenye maumivu mazito
Kwenye mioyo yao

Na sio chombo cha starehe ni walinzi wa familia zetu
Na iko wazi pia mwanamke ni mungu wa pili na ni mama zetu
Kuna muda najiuliza au mi sistahili kuwa na maisha mazuri
Au sijui kuwa haubaki kumi kwenye mia ukitoa sufuri

Kwenye mafanikio marafiki ni wengi wazito na wepesi
Mungu wangu lakini kwenye shida
I see myself I see nobody nobody else dah
Na kinachoniponza mi sio mbinafsi
Hata kipande kidogo cha mkate nataka tule wote

Lakini wao wakipata wanachotaka furaha yao Ni mi nikose
Na mi ni mtu mmoja nimeamua kuweka wazi
Ila kuna wengi mungu wangu
Wako chumbani wanajifungia wanalia kila siku
Wana maumivu na wanamwaga machozi

Verse Three – My God Lyrics by Nacha

Mungu wangu kuna watu ni vipofu hawaoni
Wakati huo huo mungu wangu wenzao wanaona
Na Wanaongezea mbwembwe za miwani machoni dah
Sina msaada kwenye dimbwa hata nikipaza sauti
Nachoambulia ni kujibiwa kila nafsi itaonja mauti

Sihofii sumu zao nitawakanyaga vichwa
Hata kama wakiamua kufumba macho kila ninapopita
Ni kama sina bahati kila nikipanga mungu haiwi
Nahitaji kusikia na unajua mi ni kiziwi
Najua mungu wangu una huruma

Mungu wangu unagawa kwa mafungu na upendeleo huna
Najiuliza ni wapi nilikwama nilikosea wapi
Au nilikuwa na radhi za mama sikukufuru ah ah
Sina maana ni kama nipo kwenye mlima mrefu pekee yangu nimesimama

Mungu umri unakwenda na matumaini yako wapi
Hata nikijilazimisha furaha sipati
Najikaza nisiwe na tamaa ingawa nimechoshwa
Na maneno yana karahaa

Nipe moyo wa subira nishinde haya majaribu
Moyo wangu una vidonda please Mungu vitibu
Natamani kuongea na mi ni bubu
Nimetengwa na marafiki mpaka na ndugu

Amani iko wapi
Duniani hakuko safi
Wengi wanakufa na stressi
Na ndoto zao kwenye nafsi

Ukingoja haki duniani unaumia
Ndio maana narudi kwako sio mbinafsi pumzi bure unanigawia
Ni kama nipo kwenye giza kinene hakuna taa wala mshumaa
Na muda wote nimesimama hakuna mahali pa kukaa

Miguu imechoka inatetemeka
Lakini nikikumbuka nilipotoka naongeza juhudi
Wakati wa mungu ni kama maji kwenye bahari
Hakuna atakayeweza kuyadeki na ikwepeki

Hukunileta kwenye hii dunia kwa bahati mbaya
Ulikuwa na makusudi na sijachoka
Unajuwa mtaji wa masikini ni juhudi
Na ningeshakuwa nimewaza kutoa kafara
Tatizo sina akili za mgando

Hadi natamani niondoke kwenye hii dunia yao
Ya majungu fitina na masimango
Nyasubi ndani ya mbanyu baby

My God Lyrics by Nacha

ALSO, SING TO – Beautiful Lyrics – Chidi Beenz

You may also like