Home GENERAL So Sad Lyrics – Young Killer Msodoki – New Song 2020

So Sad Lyrics – Young Killer Msodoki – New Song 2020

by Louis
Published: Last Updated on
So Sad Lyrics

So Sad Lyrics – Young Killer Msodoki – Download Mp3 Audio

Verse One

Ha! Naamka asubuhi yoh baby mama ananitazama
Jana usiku nilimwambia kuwa kuna pahala nimekwama
Nikaplease tuombe Mungu leo kukuche salama
Nikatafuta nimletee kabla jua halijazama

Huwaga nimeolewa ila kwa hili hajanibelieve
Kuwa nitapata like you wa jana tumelala kwa maumivu
Hatujaweza bado, till now ni miaka 15
Tuko mbali na bado haijatimia our dream

But watoto wanaenda shule ila home taabu
Elimu bure ila changamoto ni ya vitabu
Vya kujisomea hasa kiswahili na hesabu
Wife ni mgonjwa kitambo anaendelea na matibabu

Kitu inaniuma ni kulala njaa na watoto
Wakinitazama kwa huruma wanajua ni changamoto
Na mpangaji Mungu, hustle haziwezi kuwa till I die
Bado siamini ng’ombe wa maskini hazai

So lemme try, tell me
Life is so sad
Life is so sad

Verse Two

Kuna muda uko less nakosa hata mood ya mapenzi
Put God first and watch your life changing
Believe in yourself is the secret to success
But dreams mingi zinakufaga kwa stress

Dear God why hunifungulii milango
One kero za jirani anavyonishikia mabango
Zidi kunipoteza, ningewaweza ningewaharibia kitambo
Na kiukweli sina hata fedha na sijali hata pango

Please nionyeshe japo njia niweze pita
Sijapokea hata mshahara toka kwa boss mwezi wa sita
Simu zangu hashiki pia akiniona anakunja ndita
Na nyumbani hapakaliki hasa kana kwamba ni vita

Kitu inanichosha nikuwaza kesho kuna nini
Najua nguvu ndo mtaji wa masikini na ninazo
Changamoto zisituletee vikwazo
I believe mwisho wetu huwezi kuwa kama mwanzo

Trust me beiby
Life is so sad
Take me away
Ooooh yeaaah

Verse Three

Napokea simu ya home kwamba wife kazidiwa
Kajaribu kuomba msaada kwa jirani kapatiwa
Inaonekana kuna kitu kinamtesa kwenye ziwa
Sijui ni presha au ni kitu kwenye titi kafanyiwa

Kimbia Ukichelewa inaweza kuja kuwa hatari
Maana hawezi kuongea sauti inatoka kwa mbali
Kaingizwa ICU tunamngoja daktari
Tumwambie pesa mpaka uje kama atakubali

Njoo hospitali
Oooh

So Sad Lyrics Credit – Young Killer Msodoki

ALSO, SING TO – Buku Remix Lyrics – Whozu Ft Director Shaibu – New Song 2020

Related Posts