Contents
Wana Lyrics by Zuchu – Download Mp3 Audio
Verse One Wana Lyrics
Hunywi Maji yakapita
Mi nkiguna ushafika
Jina gani hujaniita baby
Ushauri hutaki kabisa
Eti uniache nina visa
Vya vifarauni na musa vingi
Nikilala naota kama unaniita
Nafumba macho navuta shuka
Naona napumbazika
Unishikapo ndipo hapo nafarijika
Mambo yako mahaba yako
Ndo maana natononoka wee
Chorus
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana aah
Verse Two Wana Lyrics
Nzi kidondani hufia wahenga walisema
Maradhi yaweza yasiwe na dawa
Kwa penzi yakapona
Rabii amenipa nusura jeuri sina tena
We ndo ganzi umenimaliza
Hasira siumwi wakisema
Nidekeze niliwaze
Washushuke wanyamaze
Nikinuna nibembeleze
Usinipepee nipulize
Watuone washtuke
Roho zao ziwaume
Mi nipike ule chote
Unenepe upendeze
Chorus
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana aah
Verse Three
Ukitaka uniweze nibebe wewe
Ukipenda unibimbe unikumbatie
Hata watu watuone wakahadithie
Nitambulishe niringe niwavimbie
Ukitaka uniweze nibebe wewe
Ukipenda unibimbe unikumbatie
Hata Lizer atuone akahadithie
Nitambulishe nitambe niwavimbie
Wana Lyrics by Zuchu
ALSO, SING TO – Dodo Lyrics – Alikiba